Picha ilipigwa 29 Juni 2005 © Thomas Hinnebusch
Zoezi la kwanza
Tangazo hili lilitolewa na Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa Kudhibiti UKIMWI.  Kabla ya kusikiliza mahojiano kuhusu tangazo hili, jibu maswali haya katika barua-pepe utakayomtumia mwalimu wako:
    
1. Tangazo linaonyesha nini?  Andika maelezo ya watu wa picha.
 
2. “Unyanyapaa” ni nomino inayotokana na kitenzi “kunyanyapaa.”  Maanake ni nini?
 
3. Chini ya picha, unaona mifano miwili ya sarufi ya dhamira tegemezi: “tusimtenge” na “aendelee.”  Kwa nini dhamira tegemezi inatumiwa katika mifano hii?
 
4. Kwa nini jina la tangazo hili ni “Unyanyapaa na UKIMWI”?  Kuna uhusiano gani baina ya mambo haya mawili?  
 
5. Ukiunganisha picha na maneno ya tangazo hili, unafikiri lengo lake ni nini?
Zoezi la pili
Sikiliza mahojiano na Bi. Janet Kaaya, Mtanzania aliyeishi Marekani.  Wakati wa kumsikiliza, fikiria maswali haya.  Unapomaliza kusikiliza, mtumie mwalimu majibu yako.
 
1. Kufuatana na Janet, msichana wa picha anaishi kwa matumaini kwa sababu gani?
 
2. Kuna tofauti gani baina ya maelezo yake Janet kuhusu picha na maelezo uliyoandika katika zoezi la kwanza?
 
3. Kwa nini Janet anasema kwamba vijana wa picha hii “ni Waafrika wa kule nyumbani”?
Zoezi la tatu
Sikiliza mahojiano ya pili na Janet.  Wakati wa kumsikiliza, fikiria maswali haya.  Unapomaliza kusikiliza, mtumie mwalimu majibu yako.
 
1. Mwanzo wa UKIMWI, watu walikuwa na mawazo gani kuhusu uambukizaji?
 
3. Kufuatana na Janet, unyanyapaa na UKIMWI uliunganishwa zaidi lini?  
 
Zoezi la nne
Sikiliza mahojiano ya tatu na Janet.  Wakati wa kumsikiliza, fikiria maswali haya.  Unapomaliza kusikiliza, mtumie mwalimu majibu yako.
 
1. Taja mifano miwili mitatu ya dhamira tegemezi katika aliyosema Janet.
 
2. Kufuatana na Janet, tangazo lina ujumbe gani kwa jamii?
 
3. Ujumbe ulioelezwa na Janet ni sawa na lengo ulilolieleza katika Zoezi la Kwanza?  
 
Zoezi la tano
Sikiliza mahojiano yote tena.  Halafu, tumia kifaa cha Springdoo urekodi maoni yako:
 
    “Bi. Janet, nakubaliana nawe kwamba ....
      Lakini sikubaliani nawe kwamba .... .”  
 
Mweleze sababu zako za kuwa na maoni haya.  Unapomaliza, mtumie mwalimu rekodi yako.